Hatimaye aliyekuwa
naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr.Asha Rose Migiro ameagwa
rasmi baada ya kumaliza mda wake katika umoja wa mataifa.Dr Migiro ametumikia
umoja wa mataifa kwa miaka mitano tangu kuteuliwa kwake mwaka 2007.
Akizungumza
wakati wa tafrija hiyo, Katibu Mkuu Ban ki Moom ameleezea baadhi ya
sababu zilizomsukuma kumteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa
msaidizi wake wa karibu.
“
Nilianza kumfahamu Asha- Rose Migiro wakati huo sote tukiwa mawaziri wa mambo
ya nje katika nchi zote. Uwezo wake na uelewa wake wa mambo ulinivutia
sana, lakini nilivutiwa zaidi pale nilipofahamu kwamba aliwahi kuwa waziri
anayehusika na masuala ya wanawake na watoto. Nikajiridhisha kwamba huyu ndiye
alikuwa ananifaa kuwa msaidizi wangu wa karibu” akasema Ban Ki Moon na kuufanya
umati ulihohudhiria tafrija hiyo kushangilia kwa nguvu.
Kama hiyo haitoshi,
Ban Ki Moon amemuelezea Dkt. Asha- Rose Migiro kama msaidizi wake wa karibu
ambaye licha ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa lakini ni mtu ambaye alikuwa
hana makuu na wala hata siku moja hakujikweza.
“ Katika kipindi chote ambacho Migiro amekuwa
msaidi wangu wa karibu, amenisaidia katika mambo mengi, ni mtu muadilifu sana,
ni mtu aliyekaribu sana na watu, aliyeamsha matumaini na kuwapa tabasamu watu
waliokuwa katika mazingira magumu. Daima amekuwa mstari wa mbele kunisaidia
na hakuna hata siku moja alipojikwenza. Na kwa sababu hii anastahili
tafrija hii” akasisitiza Ban Ki Moon.
Aidha Ban Ki Moon akamuelezea Asha- Rose
Migiro kama kiongozi ambaye daima alitoa kipaumbele cha aina yake katika
masuala ya afya ya jamii eneo alilotumia uwezo wake wote, maarifa yake
yote kama naibu katibu mkuu kupigania afya ya wanawake na watoto na watu wote
walio katika mazingira magumu
Kwa upande wao waandaaji wa tafria hiyo
na wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemuelezea Naibu Katibu Mkuu, kama
kiongozi ambaye mchango wake umesaidia sana katika kuihamasisha
jumuiya kimataifa kuweka mkazo wa aina yake katika kushughulika afya ya jamii.
Aidha Migiro
amewashukuru kwa moyo wa dhati wasaidizi wake wa karibu aliofanya nao
kazi akiwa naibu katibu mkuu na kwamba bila wao asingefika hapo alipo,
akawashukuri pia wadau mbalimbali wakiwamo mabalozi kwa ushirikiano wa hali na
mali waliompatiwa muda wote wa miaka mitano na nusu.
0 comments for "Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi umoja wa mataifa"