Latest Stories

TOP 5 Most Popular Post

Recently Comments

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kuelekea Msumbiji 0 Comments

By Unknown
Thursday, June 14, 2012 | Posted in ,

Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeagwa leo na kukabidhiwa bendera na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadick tayari kuelekea nchini Msumbiji mapema  kesho (june 15)kuikabili timu ya Taifa ya nchi hiyo (The Mambas) katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika utakaopigwa jumapili june 17.

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki ameitaka timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuiwakilisha vyema nchi katika mchezo huo. Ametoa mwito huo leo (Juni 14 mwaka huu) wakati akimkabidhi nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja, Bendera ya Taifa tayari kwa safari ya kwenda Msumbiji itakayofanyika kesho (Juni 15 mwaka huu) asubuhi. Stars itaondoka kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.

 Aidha RC amesema kiwango ambacho kilioneshwa na Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast na Gambia kimerudisha imani ya Watanzania kwa timu hiyo, hivyo kuwataka wachezaji kuendeleza moto huo.
 Aliwataka wachezaji wa timu hiyo pamoja na benchi la ufundi kupigana kiume kuhakikisha wanashinda mechi hiyo, kwani ushindi mbali ya kuwaingiza katika raundi inayofuata pia utaifanya Tanzania ipande kwenye orodha ya viwango vya ubora duniani inayotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

 Mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zampeto nje kidogo ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za huko.
 Waamuzi hao ni Hamada Nampiandraza atakayepuliza filimbi, Alberto Razafitsatamy, Paulo Andriovoavonjy na Bruno Andriamiharisoa. Kamishna wa mechi hiyo kutoka Botswana ni David Fani.

Taifa Stars inaondoka na msafara wa watu 32 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Msafara huo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Shaibu Nampunde.

Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

Leave a reply

0 comments for "Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kuelekea Msumbiji"