Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema licha ya kupewa
vitisho kumzuia asihudhurie msiba wa aliyekuwa mkurugenzi wa jiji,
Wilson Kabwe, amezingatia ubinadamu na kuweka msimamo kuwa ataendelea
kutimiza wajibu wake.
Makonda alisema hayo jana wakati wa kuaga mwili wa Kabwe kwenye ukumbi
wa Karimjee, kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake Mamba Mpinji
wilayani Same, Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayofanyika leo.
Awali, mmoja kati ya wanafamilia alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya
habari akisema kuwa familia haihitaji ushiriki wowote wa Serikali kwenye
maandalizi ya mazishi hayo.
Alitoa kauli hiyo kutokana na Kabwe kusimamishwa kazi kwa amri ya
Rais John Magufuli baada ya kusomewa makosa yake na Makonda mbele ya
umati wa watu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni.
Hata hivyo, ndugu wengine walikanusha kauli hiyo na kueleza kuwa
Serikali imekuwa ikishirikiana na familia katika kumuuguza Kabwe na
kwamba kifo chake hakikutokana na kusimamishwa kazi kwa kuwa wakati
uamuzi huo unatangazwa alishaanza kuugua.
Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Makonda aliipongeza familia ya
marehemu, akisema imevuka mtihani ambao Watanzania wengi wangeshindwa
kutokana na kulivisha tukio hilo sura ya tofauti wakati wa msiba.
“Baadhi ya watu waliniambia nisihudhurie msiba na hata baadhi ya vyombo
vya habari vikatengeneza mazingira vinayoyaona kwamba yanafaa,” alisema
Makonda.
“Ila nitaendelea kutimiza wajibu wangu na wanafamilia mmeliona hilo na niwape pongezi.”
Makonda aliwasihi Watanzania kuwa watulivu na kushauri watumishi wa umma kuwa waadilifu katika kazi zao .
“Maadam Kabwe amelala, tusitumie fursa hii kumrundikia mizigo eti
tukifikiri kwamba tutakuwa salama mbele za Mungu. Tuhakikishe kila mmoja
anafanya kwa nafasi yake na kwa wajibu wake ili tusiwatwishe mizigo
watu waliotangulia mbele za haki.”
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi za kidini,
wafanyakazi wa umma na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwamo Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Akitoa salamu za Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi),
George Simbachawene alisema kifo cha Kabwe kimewasikitisha na kwamba
ameacha pengo, si kwa familia pekee bali hata serikalini.
Source: Mwananchi
Ujumbe Huu wa Diamond kwa Bintiye Wasababisha Povu
Lakini ujumbe wake mpya kwa bintiye, Tiffah umesababisha mjadala mkubwa.
Akiweka picha ya binti yake huyo ambaye mwezi ujao anatimiza mwaka mmoja, Diamond aliandika: Buff day Girl! my little Pumpkin My Miss World @princess_tiffah kua mama, nikupe Raha ya Dunia na ujifaidie Ustar wako….. ila dah ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu, Maana ntalificha wapi hili sura langu.”
Maneno: Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu’ ndiyo yaliyosababisha povu la haja.
Hizi ni baadhi ya comments:
Twinsrebeccita: Hivi mtoto hajafikisha hata miaka miwili ushaanza kufikiria masuala yake ya ngono!!!! Maneno ya bure kwako, usitumie utupu wa mwanao kutangaza biashara yako.
Precioushamis: Mungu auTunze usichana wako /ujana wako tiffah, kinywa cha baba yako kishindwe kwa jina la yesu amina
Jahmolbiggz: Daym did u just wrote that? Any real Dad out there won’t even think of writing such words to her dota.. Shit is Crazy
Madimwashiti: @princess_tiffah never follow your parents foot steps. U need more prayer. @diamondplatnumz better pray for this little girl coz what goes around comes around. Many many little SIMBAS out there want spare you dear. That is my own thoughts. Think about it NASSEB
Neyesu Daniel: Diamond ww sio baba mwema! Utaanzaje kumwambia bint ako ivo!? Umenikera mbna unakosa madil ya kiafrika?? Acha izo bna kama ww una njia ambazo si nzur bc mfunze mwanao akue vema!
Rajabu Mussa: Tena atakua amefuata Tabia Za Huku na huku(kwa maza n baba) maana kote kote hakuna mwenye afazali…….ukila nawe utaliwaaaaa japo #Kidogo
Tuzo Hella: Atii aliwe kidogooo!!! Labda wakati anaandika hiyo post hakuwa poa!!alionja kidogo ile kitu ya Arusha inarushanga akili,coz diamond hukogi na akili mingi sasa alifikiri nn kuandika hayo maneno hayo!!eti mtt akulwe kidogo kweliii!!!! D your not serious
Unaounaje ujumbe huo?
Posted in:
feature
| Monday, July 25, 2016
Diamond Platnumz Afunguka Kulichotokea Kati Yake na Avril
Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Judith Mwangi ‘Avril’ ambaye alicheza kama video queen kwenye wimbo wa Diamond Platnumz ‘Kesho’ amefunguka na kusema hakuwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakidhani huenda kuwa Diamond Platnumz baada ya video hiyo labda alitumia nafasi hiyo kutoka naye kimapenzi
Msanii Diamond akiwa na msanii Avril kutoka Kenya |
“Diamond ni rafiki yangu ni mtu poa sana, tumejuana kwa muda mfupi lakini ni msanii mwenye bidii ya kufanya kazi na kukutana na msanii mwenye bidii ni jambo zuri, hi mtu mzuri mpole hana maneno na watu. Najua vyombo vya habari vinampa sifa nyingi tofauti na yeye lakini ukikutana na yeye moja kwa moja ni mtu mzuri sana. Baada ya kufanya ile video ya kesho hakuna project nyingine tulifanya” alisema Avril
Mbali na hilo Avril alitaja wasani watano kutoka Tanzania ambao anawakubali na kuanza na Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Raymond, Vanessa Mdee pamoja na Linah Sanga.
Posted in:
udaku
|
Misri Watangaza Kikosi Kitakachoivaa Taifa Stars
Kocha wa Misri mwenye asili ya kiajentina Hector Coper amewajumuisha kikosini wakali Mohamed Elneny na Mohamed Salah wanaovuma katika vilabu vyao kwa sasa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Taifa Stars mapema mwezi juni mwaka huu.
Kikosi kamili ni kama kifuatavyo;
Makipa: Ahmed El-Shennawy, Essam El-Hadary, Sherif Ekramy
Mabeki: Ahmed Fathi, Ahmed Hegazy, Ali Gabr, Ayman Ashraf, Hamada Tolba, Hazem Emam, Karim Hafez, Mohamed Abdel-Shafy, Rami Rabia, Sabry Rahil
Viungo: Abdallah El-Said, Amr Warda, Hossam Ashour, Mahmoud Hassan, Mohamed Elneny, Mohamed Ibrahim, Momen Zakaria, Tarek Hamed
Washambuliaji: Amr Gamal, Ahmed Hassan ‘Koka’, Marwan Mohsen, Mohamed Salah
Posted in:
michezoburudani
| Wednesday, May 25, 2016
Serengeti Boys Kusaka Nafasi Ya Tatu – 2016 AIFF Youth Cup
Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kesho Mei 25, 2016 kesho inaingia tena Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa India kukipiga na Malaysia katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu kwenye michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).
Katika mchezo wa kuwania kucheza fainali, Serengeti Boys iliruhusu sare ya mabao 2-2 Malaysia hivyo kufikisha sare ya tatu baada ya kushinda mechi moja. Serengeti Boys imemaliza hatua ya awali ikiwa na pointi sita sawa na Korea Kusini, lakini ikazidiwa bao moja hivyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ambayo Marekani iliongoza kwa kufikisha point nane.
Licha ya kuwa wenyeji, India ilitupwa mbali hivyo kwa kesho watakuwa watazamaji katika michezo yote miwili ukianzia wa Serengeti Boys na Malaysia utakaopigwa saa 7.30 mchana kwa saa za Tanzania kabla ya fainali kuchezwa saa 11.30 jioni kati ya Marekani na Korea Kusini.
India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
Posted in:
michezoburudani
|
Wema Sepetu na ‘maumivu’ ya kupata ‘Mtoto’ ameandika haya Instagram.
Wema ni staa wa filamu aliyejizolea heshima za kutosha kutokana na umahiri wake katika kazi, lakini staa huyo ‘analia’ na kukosa mtoto.
Wasanii wenzake na baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimpa faraja kila kukicha kuhusiana na swala hilo.
“Iko siku na mimi ntaitwa Mama” ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha aliyokumbatiana na mama yake.
Posted in:
udaku
|
Nay wa Mitego: Wasichana wanaopenda kukwarua waimbaji ‘Chipukizi’ ni Wolper, Nisha na Shilole.
Rapa wa shika adabu yako Nay wa Mitego, ametaja list yake ya wasanii
wa filamu wanaopenda ‘kuhondomola’ na wasanii wa Bongo flava
wanaochipukia huku wakiwa na hit radioni.
Kupitia clip ya video aliyoiweka Snapchat, staa huyo amemtaja Jackline Wolper, Nisha pamoja na Shilole.
“Kule bongo movie wasichana ambao huwa wanakwaruaga vichipukizi…kuna Wolper,kuna Nisher na Shilole….yaani wakisikia tu underground anafanya vizuri washamdaka”anasema Ney.
Kupitia clip ya video aliyoiweka Snapchat, staa huyo amemtaja Jackline Wolper, Nisha pamoja na Shilole.
“Kule bongo movie wasichana ambao huwa wanakwaruaga vichipukizi…kuna Wolper,kuna Nisher na Shilole….yaani wakisikia tu underground anafanya vizuri washamdaka”anasema Ney.
Posted in:
udaku
|
Paul Makonda: Nimezingatia ubinadamu kuhudhuria msiba wa Wilson Kabwe.
Posted in:
news
|