Latest Stories

TOP 5 Most Popular Post

Recently Comments

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

Nsajigwa, Domayo nje Yanga Kagame 0 Comments

By Unknown
Friday, July 13, 2012 | Posted in


KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga Mbelgiji Tom Saintfiet, ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaocheza michuano ya Kombe la Kagame huku nahodha wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa akiwa miongoni mwa wachezaji maarufu ambao hawataitumikia Yanga kwenye mashindano hayo.

Wachezaji wengine ambao kocha huyo amewaacha kwenye kikosi chake ni kiungo mpya aliyesajiliwa Yanga hivi karibuni akitokea JKT Ruvu, Frank Domayo na mshambuliaji chipukizi Simon Msuva kutoka Moro United na viungo Omega Sema na Nurdin Bakari ambao walikuwepo Yanga msimu uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Saintfiet alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kukaa na benchi lake la ufundi na kwamba kazi kubwa imefanyika kuwapata wachezaji hao 20 kwani kikosi chake chote ni kizuri.
Alisema anasikitika kwa wachezaji ambao hawapo kwenye kikosi cha Kagame, maana wanahitajika 20 na hawakuwa na jinsi zaidi ya kufanya vile ambavyo kanuni za mashindano zinataka.
Kuhusu Domayo, Msuva na Seme alisema bado ni vijana na anaamini wataitumikia zaidi Yanga siku za usoni na kwamba ameamua kuwaacha ili waelekeze nguvu zao katika timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 inayojiandaa kwa mashindano ya kimataifa, ambayo kwa sasa ipo kambini.
Kwa upande wa Nsajigwa alisema ni mchezaji muhimu sana katika mashindano hayo, lakini anahitaji muda wa kupumzika kwa kuwa amecheza mechi nyingi bila kupumzika kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kikosi kamili cha Yanga katika mashindano hayo yanayoanza kesho kwa Yanga kucheza na Atletico ya Burundi ni Yaw Berko, Ally Mustapha ‘Barthez’, mabeki ni Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Godfrey Taita, Oscar Joshua na Ladslaus Mbogo.
Viungo ni Stephano Mwasika, Athuman Idd ‘Chuji’, Rashidi Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan na Idrisa Rashid, wakati washambuliaji ni Hamis Kiiza, Said Bahanuzi, Jeryson Tegete na Shamte Ally.
Katika kikosi hicho pia hayupo mshambuliaji mpya wa timu hiyo Meddie Kagere aliyetangazwa kusajiliwa akitokea Polisi ya Rwanda, ambaye hata hivyo bado hajafika nchini.
Pia Tom amemjumuisha beki Kelvin Yondani aliyesajiliwa akitokea Simba hivi karibuni ingawa usajili wake umekuwa na utata baada ya Simba kudai bado ina mkataba naye.
Pia vyombo vya habari wiki hii vimeripoti kuwa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ambalo linasimamia mashindano hayo limeitaka Yanga imalizane kwanza na Simba kabla ya kumtumia beki huyo.
Yanga ndiyo bingwa mtetezi wa mashindano hayo. Licha ya kikosi hicho kocha huyo alizungumzia mchezo wa kesho na kusema utakuwa mgumu lakini watapambana kwa vile wana ushirikiano wa kutosha na kuwaomba viongozi na mashabiki wa Yanga kuachana na mawazo yaliyopita ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu na badala yake waelekeze mawazo yao kwenye Kombe la Kagame.

Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

Leave a reply

0 comments for "Nsajigwa, Domayo nje Yanga Kagame"