Latest Stories

TOP 5 Most Popular Post

Recently Comments

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI 0 Comments

By Unknown
Thursday, July 12, 2012 | Posted in ,


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amewasilisha bajeti ya Wizara yake katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma kwa kuzitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Wizara hiyo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa migogoro ya ardhi na nyumba katika maeneo ya mijini na vijijini.

Profesa Tibaijuka amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kukosekana kwa ardhi iliyopangwa na kupimwa kwa ajili ya matumizi ya mbalimbali mijini na vijijini ikilinganishwa na mahitaji pamoja na kuwepo kwa utamaduni ambao bado hauzingatii mfumo wa ubananaji wa makazi ya mijini na kasi yake vinavyolazimisha kuheshimu sheria na taratibu za mipango miji.

Aidha, Waziri wa Ardhi alisema kubadilisha utunzaji wa kumbukumbu za sekta ya ardhi kutoka mfumo usio unganishi kwenda kwenye mfumo unganishi wa ki-elektroniki ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili wizara yake.

Alisema changamoto hizi zinakwamisha uendelezaji wa dhana halisi za upangaji, upimaji na utawala wa ardhi na kuongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, serikali kupitia wizara hiyo itaendelea kujenga mfumo unganishi wa ki-elektroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za ardhi utakaowezesha upatikanaji na utumiaji wa kumbukumbu za sekta ya ardhi kwa ufanisi.

Serikali pia itaandaa mipango ya matumizi ya ardhi nchini hasa katika vijiji vilivyopo mipakani na kuendelea kutekeleza programu ya Taifa ya kurasimisha na kuzuia makazi holela mijini kwa kushirikiana na Halmashauri mbalimbali.

Alisema ili kukabiliana na matatizo ya ardhi, wizara yake itaendelea kuimarisha vyombo vya kusimamia maadili na weledi wa wataalam wa sekta ya ardhi katika ngazi zote na kuandaa utaratibu utakaowezesha mamlaka za upangaji kuweka mfumo wa udhibiti na uendelezaji wa ardhi katika ngazi ya kata.

Aidha Waziri huyo alisema wizara yake itabuni mbinu mpya za kisasa ili kupata fedha za kuendeleza shughuli za wizara nje ya bajeti kuu ya serikali na serikali za Mitaa hasa kupitia mikopo ya benki au hisa za makazi.

Profesa Tibaijuka ameliomba Bunge kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya shilingi 101,731,722,000. Kati ya fedha hizo, shilingi 10,422,891,000 ni kwa ajili ya mishahara , shilingi 71,000,000,000 ni miradi ya maendeleo na shilingi 20,308,831,000 ni kwa ajili ya matumizi mengine.

Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

Leave a reply

0 comments for "WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI"