BWAWA LA KUZALISHIA UMEME KIDATU LAZIDIWA NA MAJI
Bwawa la kuzalisha umeme kwa maji la Kidatu mkoani Morogoro limezidiwa
na maji na kulazimu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana
na Serikali kufungulia maji yaliyozidi na kuanza kupita katika geti
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.Hatua hiyo imetokana na iwapo
wataacha yaendelee kutoka bila kuyadhibiti taratibu itasababisha
uharibifu wa miundombinu na kuhatarisha maisha ya watu. Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema maji ya bwawa hilo y
amekuwa
mengi hivyo yanaweza kuathiri usalama wa bwawa, kwani limetengenezwa
kupokea kiasi fulani cha maji hivyo yakizidi presha yanagonga kwenye
kingo na yanaweza kusababisha maafa.Mramba alisema pia maji yanapotoka
katika bwawa hilo na kurudi mtoni yanaweza kusababisha madhara kwa
wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali kwenye mto, hivyo ni vema
kuyadhibiti.Alisema bwawa hilo limefurika maji licha ya kuzuia maji ya
bwawa la Mtera yanayoingia humo kufungwa kwa zaidi ya wiki mbili na
mashine zote nne za kuzalisha umeme kuendelea kuzalisha umeme kwa
kiwango cha juu.
0 comments for " "