Latest Stories

TOP 5 Most Popular Post

Recently Comments

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

FFFFFFFFFFFFF

FFFFFFFFFFFFF
XXXXXXXXXXX

KANUMBA KAACHA MADENI 0 Comments

By Unknown
Monday, June 11, 2012 | Posted in ,

CHANZO CHA HABARI: IJUMAA WIKIENDA


Wakati kukiwa na malumbano kati ya wazazi juu ya mali alizoacha marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, mama mzazi wa staa huyo, Flora Mtegoa ametoboa siri kuwa baba Kanumba, mzee Charles Kusekwa aache chokochoko kwani mwanaye kaacha madeni kibao, Ijumaa Wikienda limezungumza naye ana kwa ana.
Flora alifunguka kuwa mwanaye Kanumba alikufa maskini japokuwa baba yake amekuwa akidai mali kwa nguvu bila kujua mwanaye huyo anadaiwa madeni mengi ambayo kwa sasa wamesitisha kuyalipa kwanza kupisha suala la mirathi ndipo zoezi la kulipa madeni lifuate.
“Jamani Kanumba hakuwa na utajiri mkubwa kama baba Kanumba anavyosema kwani madeni yapo mengi ikiwa ni pamoja na nyumba aliyokuwa anaishi, ofisi za kampuni yake ya The Great Films na mengine ambayo siwezi kuyaweka hadharani mpaka mahakamani siku ya mirathi.
“Yaani kila ninachokipata kinapita tu hakikai mkononi sijui niseme nini ili baba Kanumba anielewe,” alisema Mama Kanumba kwa uchungu.
Mzazi huyo wa marehemu Kanumba aliendelea kubumburua kuwa amekuwa akimshangaa baba Kanumba kupiga kelele kuhusu mali hivyo kama yupo tayari kulipa madeni yote hayo yeye yuko tayari kujiweka pembeni ili ashughulikie hilo suala kwa sababu yupo katika wakati mgumu kwa sasa.
Hata hivyo, mama Kanumba alisema suala la mirathi kila kitu kimekamilika na familia imemteua yeye kusimamia hivyo wakati wowote atatinga mahakamani kwa ajili ya kufungua mirathi ili madeni hayo yalipwe.




BABA KANUMBA KAMA KAWA
Baada ya mazungumzo marefu yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kanumba maeneo ya Sinza Vatican anakoishi mama huyo, Ijumaa Wikienda lilimwendea hewani baba Kanumba na kumweleza hayo yote ambapo kama kawaida yake alifunguka:
“Huyo mama Kanumba aache hizo, najua ni visingizio tu, kwa taarifa yake fedha alizokabidhiwa niliziona. Zinatakiwa kwenye miradhi. Mama Kanumba aache hizo.”

KWA NINI?
Kauli ya mama Kanumba inakuja kufuatia baba Kanumba kudai kuwa anachojua ni kwamba mwanaye ameacha nyumba ya gorofa, Sh. milioni 150 benki, kampuni na viwanja vitatu hivyo anavihitaji kutoka kwa Flora anayevishikilia.

Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

Leave a reply

0 comments for "KANUMBA KAACHA MADENI"