CHANZO CHA HABARI: GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA
Wakati leo utata wa umri na jina la Elizabeth Michael ‘Lulu’ ukijulikana kupitia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ili kupisha kesi ya kifo cha Steven Kanumba kuanza kusikilizwa, Ijumaa Wikienda limesikia kilio cha staa huyo na mwenzake, Kajala Masanja kuwa kwa maisha wanayoishi kwa sasa bora wafe.
Kwa mujibu wa chanzo kilichokwenda kuwatembelea mastaa hao hivi karibuni kwenye Mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar ambacho ni msanii mkubwa wa filamu, wawili hao wamechoshwa na maisha ya kukaa nyuma ya nondo hivyo wanamuomba Mungu kesi zao ziishe ili wajue moja kuliko kuendelea kusota bila kujua hatima yao. “Waliniambia kwa jinsi walivyozoea maisha ya uraiani na kwa hali ilivyo bora nao wamfuate Kanumba (marehemu Steve),” alisema staa huyo.
LULU
Katika kesi ya Lulu, mawakili wa utetezi waliiomba mahakama ufanyike uchunguzi wa umri wa mteja wao huku wakipinga umri wa miaka 18 ulioandikwa kwenye maelezo ya kesi ili kama ni chini ya hapo ikasikilizwe mahakama ya watoto hivyo kila kitu kitajulikana leo.
KAJALA
Kajala na mumewe Faraja Chambo wanaendelea kusota rumande baada ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yao, Sundi Fimbo kwenda likizo ya uzazi ya miezi mitatu ambapo wamekuwa wakifikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu na kesi yao kuishia kutajwa tu hadi hakimu huyo atakapomaliza likizo.
Kajala na mumewe wanakabiliwa na mashtaka matatu kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na kutakatisha fedha haramu.
0 comments for "LULU: BORA TUFE"