TUZO za
kwanza kabisa za waigizaji wa filamu zimepangwa kufanyika mwezi ujao, ikiwa ni miezi michache baada ya kifo cha muigizaji Steven Charles Kanumba. Mratibu
wa kampuni ya Bantu Film Award, Stuart Kambona amesema kuwa hatua ya kuanzisha tuzo hizo inatokana na muitikio wa soko la
filamu za Tanzania kwa hivi sasa tofauti na awali. Alisema kuwa Watanzania
wengi walikuwa wanapenda zaidi filamu za kigeni na kufunika zile za
hapa nyumbani.
Alisema
kuwa kutokana na mapinduzi yaliyofanywa na wasanii wa fani hiyo, filamu za
Tanzania kwa sasa zina soko la hali ya juu na imtokana na tabia ya watanzania
kubadili mwelekeo. Alisema kuwa ili kuhakikisha Tanzania inafikia hatua ya
Hollywood, wameamua kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya vizuri na
kuifikisha fani hiyo katika hatua ya sasa.
“Tunaamini
kuwa kupitia tuzo hizi, waigizaji au wasanii wa filamu watatengeneza filamu
zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kutwaa tuzo na soko kwa ujumla, tunaamini
tutafikia lengo letu japo tumebakisha muda mfupi mpaka tuzo zenyewe
kufanyika,” alisema Kambona.
Alisema
kuwa kwa kuanzia watashindanisha filamu zote za Tanzania ambazo kwa sasa zipo
sokoni ili kutoa fursa kwa kila msanii wa fani hiyo
kushindana. Jumla ya tuzo 28 zitashindaniwa kwa mwaka huu.
Baadhi ya
tuzo hizo ni Filamu Bora, Muongozaji Bora, Muigizani Bora mkuu wa Kiume,
Muigizaji Bora Mkuu wa Kike, Msaidizi Bora Mkuu msaidizi wa kike na wa kiume,
msanii chipukizi bora, filamu ya asili, Mpiga picha bora, Best Sound Track,
Best Make-Up artist, Best Costume Designer, Best Documentary, Best Visual
effect, best Film editor, best script na Tuzo ya Heshima.
Tuzo
nyingine ni Outstanding Pioneer, Best Comedian, Best Cover Design, Best
producer, Best Distributor, Best Action Movie, Best African Film outside
Tanzania, Best Ligting, Best Sound na Best Story.
Muigizaji
nyota wa kike nchini, Irene Uwoya aliwapongeza waandaaji hao kwa kuanzisha tuzo
hizo ambazo alisema zitawapa changamoto kwao kuandaa filamu za ushindani.
Alishukuru
kampuni ya Bantu kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo anaamini zitawafanya
kuandaa filamu zenye ubora wa hali ya juu.
"Tuzo
hizi zitatufanya tufanye kazi nzuri zaidi ili kuingia katika ushindani, natoa
wito kwa waigizaji wenzangu kufanya kazi kwa umakini ili kuleta msisimko na
ushindani zaidi," alisema Uwoya.
Muigizaji Mkongwe,
Jacob Steven (JB) alisema kuwa anaamini tuzo hizo zitawafikisha pale ambao wao
wamekusudia na vile vile kuibua vipaji vingine katika tasnia hiyo.
JB alisema
kuwa tuzo hizo zitawafanya mashabiki wao kujua undani wa fani yao kwa kuwajua
watunzi bora, wapiga picha bora na wengineo.
0 comments for "Miezi michache baada ya kifo cha Kanumba,tunzo za wasanii bora wa filamu kuanza kutolewa."