Itakumbukwa
tu kuwa mapema wiki hii Mh. Raisi JK alifanya
ziara nchini Uingereza kuudhulia na kuhutubia mkutano wa kimataifa wa viongozi
kujadili Uzazi wa mpango kwa nchi maskini zaidi duniani,Mkutano huo ulifanyika
nchini Uingereza katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July
11,2012.
Mkutano huu uliandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Uingereza na Mfuko wa Bill na Melinda Gate pamoja na wadau wengine.
Hata hivyo ,tutakumbuka kwamba mwishoni mwa
mwaka 2011 waziri mkuu wa Uingereza wakati akihutubia mkutano wa jumuiya
ya madola Perth,Australia alitoa masharti kwa nchi yoyote inayotaka msaada kwamba ni lazima ziruhusu ndoa ya jinsia moja yaani “ushoga”.
SWALI:
Kwa kuwa
mkutano huu unalenga kuzisaidia nchi masikini zaidi duniani katika harakati za
uzazi wa mpango,na nchi nyingi masikini zipo
katika bara la Afrika.Je hii siyo adhma ya serikali ya Uingereza kupenyeza
siasa zake za ndoa ya jinsia moja katika nchi hizi maskini?
0 comments for "Je ziara ya JK Uingereza ni harakati za David Cameroon kushawishi ushoga nchi maskini?"