SIKU chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema
Isaac Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa
huku gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR
likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio hilo
lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake
Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani
kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.
KIKWAZO CHA NGUVU
Hata hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti,
majambazi hayo yalishindwa kuingia ndani kabisa kutokana na milango
madhubuti iliyopo kwenye nyumba hiyo ya kisasa.
WAJIPOZA KIDOGO
Kule ndani ya geti, walivunja mlango wa gari hilo
na kuiba vitu mbalimbali kama kifaa cha kudhibiti mwenendo wa umeme
ndani ya gari (control box), vifaa vya kufungulia vioo, milango na
madirisha (power window) na vioo vinavyomuongoza dereva kuona nyuma
(side miller).
Vitu vingine ambavyo viliambatana na wizi huo ni
‘makapeti’ ya ndani na vitu vingine vidogovidogo ambavyo vilikuwa ndani
ya geti hilo.
WEMA AWASHANGAA WALINZI WAKE
Akielezea mazingira ya tukio hilo,
Wema alisema kuwa hata yeye ameshangazwa na uvamizi huo ambao umemfanya
kuibua maswali mengi kuliko majibu hasa akizingatia kuwa tukio hilo
limetokea wakati nyumba yake ina walinzi wawili.
“Ni kweli nimeibiwa
hivyo vitu kwenye gari na vingine vilikuwa nje, ila mazingira ya
kuvamiwa na yale majambazi yananitia shaka sana maana walinzi wangu
wawili walikuwepo muda wote, sasa sijui nini kilitokea?” alisema Wema
kwa sauti ya kupooza.
Akaendelea: “Sikuwa na namna kwao, nilikwenda
kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ili angalau nisaidiwe
utatuzi wa jambo hili sambamba na kuwabananisha walinzi wangu ambao
walikuwepo usiku wa tukio.
“Naamini kama geti la kutokea nje
lingekuwa legelege, wangeiba na gari lenyewe. Lakini hili geti ni gumu,
mpaka kulifanya lifunguke wangeweza kuchukua masaa matano ambapo
kungekuwa kumekucha.”
INAWEZEKANA SABABU IKAWA HII?
Katikati ya Juni mwaka huu, staa
huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, alitangaza kupitia runinga kwamba
anamiliki nyumba hiyo huku akisema ina kila kitu ndani.
Kwa mujibu
wa picha zilizoenea kwenye mitandao mbalimbali Bongo, sebule ya nyumba
hiyo inaweza kushawishi ‘wazee wa kazi’ kunyatia kwani Meneja wa Wema,
Martin Kadinda alisema manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na samani zake
shilingi Milioni 4OO ‘ziliteketea’.
HABARI ZA KIPOLISI ZATHIBITISHA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi,
Kinondoni, Charles Kenyera hakupatikana siku ya Jumanne kuzungumzia
tukio hilo licha ya kwamba, habari za kipolisi zilithibitisha Wema
kukumbwa na uvamizi wa watu wanaodhaniwa ni majambazi.
Latest News!
Advertisement![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s_g23otZ0Nq2MOkoX2AhxGLaiWqmIePJMsFK3sP8islSRSi53V0U533D1aQ-a_WCGq77cDVCkQcKOF3ElQ3WHvStPzh1AA1xWRqQ42xIjPlI_s0wQHoTHl=s0-d)
Related Posts
WIZI MTUPU!!