ALI KIBA JUSTINE BIEBER HAKUUTENDEA HAKI WIMBO,JE NI WIMBO GANI?
Msanii wa bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kusema kuwa anauzimia sana wimbo wa What do you mean wa msanii Justin Bieber kwa vile ambavyo umetengenezwa na sauti inasikika kuliko vile Beiber alivyoimba na kutamani wimbo huo ungeangukia mikononi mwake.
Kiba aliyasema hayo kwenye kipindi cha Playlist cha Times Fm alipotakiwa kuchagua wimbo wa kusikiliza ndipo alipouchangua wimbo huo na kutoa sababu hizo.
“napenda sana track hii jinsi ilivyo prodyuziwa kwa sababu sound naiskia vizuri sana kiukweli japokuwa ameimba lakini naweza kusema ameimba sio ile ki mature zaidi (kikomavu) ,ameimba ki teenage fulani..I wish ningeipata mimi” alisema Kiba.
Source: Times fm
0 comments for "ALI KIBA JUSTINE BIEBER HAKUUTENDEA HAKI WIMBO"