MAMBO yanaonekana kutotulia kuhusiana na beki Kelvin Yondani iwapo
ataichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza
Julai 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kanuni za
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), zinasisitiza
lazima mchezaji awe na leseni aliyoitumia katika ligi kuu ya nchi yake
au iliyoidhinishwa na shirikisho lake.
Yondani ana leseni ya Simba
kwa kuwa ndiyo aliyoitumikia msimu uliopita, kuhusiana na Yanga, bado
TFF haijamuidhinisha kwa kuwa Simba inasisitiza ni mchezaji wake na
imeshawasilisha mkataba katika shirikisho hilo.
Katibu Mkuu wa
Cecafa, Nicholas Musonye, amesisitiza utaratibu kufuatwa kabla ya
mchezaji yeyote kuanza kuitumikia klabu katika Kagame.
“Lazima kila
mchezaji awe na leseni katika Kagame, iwe imeidhinishwa na shirikisho
lake. Tusingependa kuona kuna malumbano baada ya kuanza kwa michuano.
“Kama kuna mchezaji mgeni, basi klabu zihakikishe zimemalizana na taratibu zote zimefuatwa,” alisema Musonye.
Kwa
Yondani, TFF italazimika kulimaliza suala lake ikiwezekana kwa
kuzikutanisha klabu hizo au kufuata taratibu kwa kuangalia mikataba na
kama ule wa Simba utakuwa ni halali, basi itakuwa vigumu beki huyo
kuitumikia Yanga katika Kagame.
Wakati huohuo, TFF imezionya klabu za
Tanzania Bara kwa kuzitaka zitumie wachezaji waliosajiliwa tu, ambao
watashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.
Katibu Mkuu wa TFF,
Angetile Osiah, amezitaka klabu za Yanga, Simba na Azam zinazoshiriki
michuano hiyo, kuhakikisha haziitumii vibaya michuano ya Kagame kwa
kuwajaribu wachezaji kabla ya kuwasajili.
“Tunazitaka klabu shiriki za Simba, Yanga na Azam kutotumia michuano hii kwa ajili ya kuangalia wachezaji kabla ya kuwasajili.
“Zihakikishe kuwa wachezaji zitakaowatumia ni wale ambao tayari zimewasajili kwa ajili ya kuwatumia kwenye ligi,” alisema Osiah.
Mohammed
‘Meddie’ Kagere na Yondani ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na
Yanga hivi karibuni na majina yao bado hayajapitishwa na TFF, wakati
Patrick Nkanu, Lino Musombo ni kati ya nyota waliotua Msimbazi wiki
kadhaa zilizopita.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi, ndiyo
watakaofungua pazia la michuano ya Kagame kwa upande wa timu za
Tanzania, kwa kuivaa Atletico ya Burundi jioni ya Julai 14 kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar.
Latest News!
Advertisement
Related Posts
YONDANI KUKOSA KAGAME? 2 Comments
By UnknownWednesday, July 11, 2012 | Posted in
feature,
michezoburudani
Leave a reply
CECAFA fuateni sheria acheni usimba na uyanga
This comment has been removed by the author.